International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumapili August 31 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
31 Aug 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumapili August 31 2025

Tottenham Hotspur wanaongoza mbio za kumsajili beki wa Manchester City Manuel Akanji, mwenye umri wa miaka 30, wakilenga kuwazidi ujanja AC Milan na Crystal Palace kupata sahihi yake. (Gazetta Dello Sport)

Kocha mkuu wa Barcelona Hansi Flick amesema anaamini kuwa kiungo mshambuliaji mwenye umri wa miaka 22 Fermin Lopez, ambaye ameichezea Hispania mara mbili, hataondoka klabuni hapo katika dirisha hili la usajili licha ya kuhusishwa na Chelsea. (ESPN)

Lakini Chelsea wako tayari kutoa ofa nono kwa ajili ya Lopez, ambaye thamani yake Barcelona ni euro milioni 90 (Β£78m). (Mundo Deportivo) West Ham wameingia katika mbio za kumsajili Fabio Vieira kutoka Arsenal, lakini Stuttgart na klabu nyingine kubwa ya Bundesliga pia wanavutiwa na kiungo huyo Mreno mwenye umri wa miaka 25. (Sky Sports Germany)

Beki wa Manchester United na Morocco Noussair Mazraoui, mwenye umri wa miaka 27, anasakwa na klabu ya Serie A, Juventus. (Gazetta Dello Sport - in Italian)

RB Leipzig wanamnyemelea kiungo wa Liverpool na timu ya taifa ya England U21 Harvey Elliott, mwenye umri wa miaka 22, kama mbadala wa Xavi Simons, lakini klabu hiyo ya Ujerumani bado inasita kufikia dau linalohitajika na Liverpool. (ESPN)

Liverpool wanaweza kuhamia kwa kiungo wa Aston Villa na England Morgan Rogers, mwenye umri wa miaka 23, iwapo uhamisho wa Elliott utafanikiwa. (Football Insider)

Winga wa Brazil Rodrygo, mwenye umri wa miaka 24, ataendelea kubaki Real Madrid katika dirisha hili la usajili licha ya klabu kadhaa ikiwa ni pamoja na Liverpool na Arsenal kuonyesha nia ya kumsajili. (Marca)

Leeds United bado wanavutiwa na kiungo mshambuliaji wa Leicester City na Morocco Bilal El Khannouss, mwenye umri wa miaka 23, baada ya uhamisho wao wa Facundo Buonanotte kutoka Brighton kukwama. (The Athletic)

Chelsea wako tayari kutekeleza kipengele cha mkataba cha kuuzwa kwa mshambuliaji wa Braga Roger Fernandes, mwenye umri wa miaka 19, kabla ya dirisha la usajili wa majira ya kiangazi kufungwa. (A Bola)

Aston Villa wanatarajia kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 21.25 kwa ajili ya beki wa kati wa Osasuna na Cameroon Enzo Boyomo, mwenye umri wa miaka 23, huku kocha Unai Emery akitaka kuimarisha safu yake ya ulinzi. (The Telegraph)

Klabu mbili za Ligi Kuu ya England zina hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Sevilla na timu ya taifa ya Ubelgiji Dodi Lukebakio, mwenye umri wa miaka 27, huku klabu hiyo ya Hispania ikijiandaa kupokea ofa kabla ya siku ya mwisho ya usajili. (Fabrizio Romano)

BBC

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
6h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
10h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
11h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
13h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
16h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
16h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
16h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
18h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
22h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’