International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Septemba 1 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1 Sep 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Septemba 1 2025

Liverpool wamekubaliana ada ya Β£125m na Newcastle kumsajili Alexander Isak. The Reds watawasilisha ada ya rekodi ya Uingereza itakayofikia Β£130m. (Telegraph)

Aston Villa wamefanya mazungumzo na Manchester United kuhusu usajili wa winga wa England Jadon Sancho, 25. (Athletic)

Aston Villa pia wamewasilisha nia ya kumsajili kipa wa Kibelgiji wa Royal Antwerp, Senne Lammens, 23. (Fabrizio Romano) Bayern Munich wameondoa ofa yao kwa mshambuliaji wa Chelsea na Senegal Nicolas Jackson, 24. (Florian Plettenberg)

Tottenham wamewasiliana na Atalanta kuhusu usajili wa winga wa Nigeria Ademola Lookman, 27, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Bayern Munich. (Sky Sports Germany)

Galatasaray wako kwenye mazungumzo na Tottenham kuhusu dili la kumsajili kiungo wa Mali Yves Bissouma, 29. (Independent)

AC Milan wamewasilisha ofa rasmi ya kumsajili kiungo wa England wa Liverpool, Joe Gomez, 28, kwa mkataba wa kudumu, huku vilabu vikiwa kwenye mazungumzo. (Fabrizio Romano)

Fenerbahce wanataka kukamilisha dili la kumsajili kipa wa Brazil Ederson, 32, kutoka Manchester City baada ya wapinzani wao wa Uturuki Galatasaray kukataliwa ofa ya euro milioni 10 (Β£8.7m). (Fabrizio Romano)

Newcastle United wanataka kumsajili mshambuliaji wa Ukraine wa Roma Artem Dovbyk, 28, kwa mkopo wenye kipengele cha kumnunua moja kwa moja kwa ada ya Β£30m. (Sun)

Aston Villa wamekubaliana na Aberdeen kumsajili kiungo wa kati wa timu ya vijana ya Scotland Fletcher Boyd, 17. (Football Insider)

Kikosi cha Unai Emery, Aston Villa, pia kiko karibu kumsajili beki wa Kiswidi Victor Lindelof, 31, ambaye yupo huru baada ya kuondoka Manchester United mwishoni mwa mkataba wake. (Birmingham Live)

BBC

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
4m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
33m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’