Local,Normal News,Azam

Ibenge apania makubwa ligi kuu 2025/26

Joel JJ By Joel JJ
1 Sep 2025
Ibenge apania makubwa ligi kuu 2025/26

Kocha Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge amesema timu yake bado inaendelea kujifua kwa ushindani na itakuwa tayari siku ya mechi ya kwanza ya michuano iliyo mbele yao.

Azam Fc inatarajia kuvaana na Al Merrikh Bentiu ya Sudan Kusini katika Kombe la Shirikisho Afrika mechi ambayo imepangwa kuchezwa Septemba 19 na marudiano ni Septemba 26 katika mechi za awali za mashindano hayo ambapo itaanzia ugenini.

Ibenge ameyasema hayo muda mfupi baada ya kuambulia suluhu dhidi ya Vipers katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa kwa Azam FC ambayo imeweka kambi ya kujiandaa na msimu nchini Rwanda.

Akizungumzia maandalizi hayo, Ibenge alisema timu yake inaendelea kujengeka siku hadi siku na kumpa wakati wa kubadilika kwenye mifumo ili kujenga timu bora na yenye ushindani ndani na kimataifa.

“Sio mbaya bado tunaimarika kulingana na mechi tunazocheza timu inaendelea kufanya vizuri kwa kuingia kwenye mifumo yangu wachezaji wataendelea kujifua kidogo kidogo watakuwa tayari siku ya mchezo wa kwanza”

“Kwa mujibu wa mechi tulizocheza tukiwa huku tulianza mdogo mdogo sasa tunaendelea kuimarika nafikiri suala la utayari kwa wachezaji ni mapema sana kusema ila utayari utaonekana siku moja kabla ya mechi ya mashindano,” Ibenge alinukuliwa na Mwanaspoti

Akizungumzia ratiba alisema ameiona na anaziheshimu timu watakazokutana nazo, lakini kwa sasa wanaendelea kujifua kwa ajili ya mashindano yote yaliyo mbele yao kwa lengo la kusuka kikosi cha ushindani.

“Ratiba nimeiona naendelea kujenga timu yangu utayari bado, mechi zote zilizo mbele yangu ni sawa. Kinachotakiwa ni utayari na ushindani jambo ambalo naamini litafanyika muda ukifika.”

 Kikosi hicho kikiwa nchini Rwanda kimecheza mechi dhidi ya Polisi FC na kutoka sare ya bao 1-1, ikachapwa 1-0 na AS Kigali, ikashinda mabao 2-0 dhidi ya APR FC, na suluhu dhidi ya Vipers.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
6h ago
READ MORE →
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
10h ago
READ MORE →
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
11h ago
READ MORE →
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
13h ago
READ MORE →
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
16h ago
READ MORE →
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
16h ago
READ MORE →
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
16h ago
READ MORE →
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
18h ago
READ MORE →
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
22h ago
READ MORE →
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE →