International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano Septemba 03 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Sep 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano Septemba 03 2025

Marc Guehi hajafurahishwa sana na Crystal Palace kwa kumnyima uhamisho wa Β£35m kwenda Liverpool, ambayo ilikuja baada ya meneja Oliver Glasner kutishia kujiuzulu ikiwa beki huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 25 atauzwa. (Guardian)

Kama Liverpool wangetoa pauni milioni 55 kwa Guehi basi Crystal Palace wangeendelea na uhamisho huo na huenda Reds wakakabiliwa na ushindani kutoka kwa Real Madrid kumsajili bila malipo. (Telegraph – Subscription Required)

Guehi, katika mwaka wa mwisho wa kandarasi yake ya Crystal Palace, atakataa ofa yoyote ya mkataba mpya huku akipanga kuondoka kama mchezaji huru msimu ujao wa joto. (Time – Subscription Required)

Manchester United ilitaka kumnunua tena Danny Welbeck kutoka Brighton kwa mwaka wa pili msimu huu wa joto, lakini mmiliki mwenza Sir Jim Ratcliffe hakuidhinisha uhamisho wa mshambuliaji huyo wa zamani wa Uingereza mwenye umri wa miaka 35. (Athletic – Subscription Required)

Manchester United bado iko tayari kumuuza mlinda lango wa Cameroon Andre Onana, 29, katika siku zijazo, huku madirisha ya uhamisho nchini Uturuki na Saudi Arabia yakiwa kati ya yale ambayo bado yamefunguliwa. (Team-Talks)

Nottingham Forest inatazamiwa kumsajili kiungo wa kati wa England chini ya umri wa miaka 17, Chinaza Nwosu, 17, kutoka West Ham, baada ya kushinda ushindani kutoka kwa vilabu vingine vikuu. (Fabrizio Romano,)

Tottenham ina matumaini ya kumuuza kiungo wa kati wa Mali Yves Bissouma, 29, kwa klabu katika nchi ambayo dirisha la usajili bado halijafungwa. (Subscription Required)

Aston Villa wanafurahia kuendelea na Emiliano Martinez msimu huu licha ya mpango wake wa kuhamia Manchester United kutotimia, na kipa huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 33 hataki kujiunga na Ligi Kuu ya Uturuki. (Fabrizio Romano, )

Aston Villa walikuwa wamekubali dili la thamani ya zaidi ya ofa ya Manchester United ya pauni milioni 18.1 kumsajili kipa wa Royal Antwerp Senne Lammens, lakini Mbelgiji huyo mwenye umri wa miaka 23 aliwapuuza Villans hao kuhamia Old Trafford. (Mail - Subscription Required)

Siku ya mwisho ya kuhama kwa Yoane Wissa kutoka Brentford hadi Newcastle ilikamilishwa zikiwa zimesalia sekunde 30 tu, baada ya mshambuliaji huyo wa DR Congo mwenye umri wa miaka 29 kushindwa kusaini moja ya fomu hizo. (Sky Sports, )

Mabingwa wa Uskoti Celtic wamefanya mawasiliano na Patrick Bamford, ambaye aliondoka Leeds United mwezi huu, katika jitihada za kumsajili mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 31 kwa uhamisho wa bure. (Herald - Subscription Required)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
37m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’