Klabu ya Yanga ina thamani ya Shilingi Bilioni 100, baada ya kamati maalum iliyoundwa kwa ajili ya tathmini hiyo kukamilisha kazi yake.
Akizungumza jana katika Mkutano Mkuu wa Wanachama uliofanyika kwenye ukumbi wa SuperDome, Masaki jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Alex Mgongolwa, alisema tathmini hiyo imefanywa na kampuni ya kimataifa ya ushauri wa uwekezaji na mali isiyohamishika, Colliers International.
Mgongolwa alisema hatua hiyo ni mwanzo wa mchakato mpana wa klabu kuingia katika mfumo wa kisasa wa uendeshaji kwa kuuza hisa, na kuongeza kuwa thamani hiyo itatumika kama mwongozo katika taratibu zote za uwekezaji zitakazoanza hivi karibuni.
Aidha, katika Mkutano huo wa Wanachama, ilisomwa taarifa ya mapato na matumizi kwa msimu uliopita 2024/25 naย ikasomwa bejeti ya klabu kwa msimu ujao 2025/26
Akisoma taarifa ya mapato na matumizi ya klabu, Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji alisema mapato ya klabu kwa msimu uliopita ni Tsh Bilioni 25.6 huku matumizi yakiwa Tsh Bilioni 25.3 kukiwa akiba ya takribani laki 3
Aidha Bajeti ya Yanga kwa msimu ujao 2025/26 ni Tsh Bilioni 33.6