International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne Septemba 16 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Sep 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne Septemba 16 2025

Mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland amekuwa kivutio kikuu kwa rais wa Barcelona Joan Laporta, ambaye ana uhakika mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway, 25, atajiunga na klabu hiyo ya La Liga siku zijazo. (El Nacional - In Spanish)

Manchester City wako tayari kushindana na Liverpool kwa ajili ya kumsajili bila malipo mlinzi wa England na Crystal Palace Marc Guehi mwenye umri wa miaka 25 msimu ujao, mkataba wake utakapokamilika. (Mirror)

Brentford wameonyesha nia ya kutaka kumnunua beki wa pembeni wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 19 Almugera Kabar. (Bild - In Deutch, Subscription Required)

Everton itakataa mbinu zozote za kumnunua beki wa kati wa England Jarrad Branthwaite 2026 huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 akiwa sehemu ya mradi wa muda mrefu katika klabu hiyo. (Talksport)

Skauti kutoka Arsenal, Chelsea, Manchester United, Barcelona na Real Madrid wote wamekuwa wakimtazama kiungo wa kati wa Ajax na Ubelgiji Jorthy Mokio mwenye umri wa miaka 17. (Caughtoffside)

Kiungo wa kati wa Crystal Palace na England Adam Wharton, 21, ana nia ya kutaka kujiunga na Liverpool licha ya kutakiwa na Real Madrid, Chelsea na Manchester United. (Fichajes - In Spanish)

Mgombea urais wa Benfica Cristovao Carvalho anasema kuwa atamfukuza kocha Bruno Lage na kujaribu kumshawishi kocha wa zamani wa Liverpool Jurgen Klopp kuchukua nafasi yake iwapo atachaguliwa mwezi ujao. (Sportbild - In Germany)

Mgombea mwingine wa urais wa Benfica Joao Noronha Lopes anataka kumrudisha kocha wa Manchester United Ruben Amorim katika klabu hiyo ya Lisbon, ambako alikaa miaka tisa kama mchezaji. (Times - Subscription Required)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’