Kikosi cha Yanga leo kinarejea mazoezini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Pamba Jiji ambao utapigwa Jumatano, Septemba 24 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Msimu huu Yanga imechagua kutumia dimba la Mkapa kama uwanja wake wa nyumbani katika mechi za ligi kuu, kombe la CRDB na Ligi ya mabingwa
Ni baada ya Serikali kufungua uwanja huo ambao kwa takribani misimu miwili haukutumika kwa mechi za ligi kutokana na ukarabati uliokuwa ukiendelea
Mabingwa hao wa ligi kuu kwa misimu minne mfululizo, wataanza kulisaka taji la tano mtawalia katika mchezo huo ambao utapigwa saa 1 usiku
Yanga kurejea dimba la Mkapa ni habari njema kwa mashabiki ambao sasa watapata nafasi ya kuishuhudia timu yao kwa wingi
Katika misimu miwili iliyopita, Yanga ilitumia viwanja vya Azam Complex na KMC Complex ambavyo vilichukua idadi ndogo ya mashabiki wasiozidi 7000
