Leo ni siku kubwa kwenye dunia ya soka ambapo Tuzo za Ballon dβOr zinatolewa kwa vipengele mbalimbali, zikihusisha mastaa wakubwa wanaowakilisha vilabu na mataifa tofauti.
Hata hivyo, habari kubwa imeibuka β Paris Saint-Germain (PSG) haitokuwepo kwenye sherehe hizo licha ya kuwa na wachezaji 10 walioteuliwa (nominees).
Sababu kuu ya PSG kukosa hafla hiyo ni ratiba ya ligi. Timu hiyo itakuwa uwanjani kucheza mechi ya Ligi 1 dhidi ya Marseille, pambano kubwa la kisoka nchini Ufaransa. Awali, mechi hii ilipangwa kuchezwa jana, lakini kutokana na changamoto za hali ya hewa, iliahirishwa na kupangwa upya leo β muda sawa na utoaji wa tuzo hizo za kifahari.
Hali hii imeweka PSG katika nafasi ngumu. Kwa upande mmoja, Tuzo za Ballon dβOr ni heshima binafsi kubwa kwa wachezaji, na PSG kuwa na nominees 10 ni rekodi inayoongeza hadhi ya klabu hiyo.
Kwa upande mwingine, pambano la Marseille ni Clasico ya Ufaransa, moja ya michezo mikubwa zaidi kwenye kalenda ya Ligue 1, na lina umuhimu mkubwa kwa mashabiki na hatma ya msimu.
Kutokuwepo kwao Paris kwenye jukwaa la Ballon dβOr kunaweza kuibua hisia mseto. Wachezaji wanaotegemewa kuibuka na tuzo, au hata kuingia kwenye orodha fupi ya juu, watakosa sherehe hiyo ya kihistoria. Hata hivyo, wengi watabaki na faraja kwamba tuzo hizo hutolewa kwa heshima binafsi na si lazima uwepo ili kushinda.
Kiungo mshambuliaji wa PSG Ousmane Dembele ni miongoni mwa wanaopigiwa chapuo kushinda tuzo hiyo