Local,Normal News,Simba

Simba kuivaa Gaborone United bila mashabiki

Joel JJ By Joel JJ
β€’
26 Sep 2025
Simba kuivaa Gaborone United bila mashabiki

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amethibitisha kuwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Gaborone United ambao utapigwa Jumapili, Septemba 28 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, hautahudhuriwa na mashabiki

Ahmed amesema Simba imeadhibiwa na CAF kutokana na matukio ya mashabiki kuvamia uwanja na kuwasha fataki ambazo zimepigwa marufuku msimu uliopta katika mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho (CAFCC) dhidi ya Al Masry

Ahmed amewaasa mashabiki wa Simba kuepuka matukio ya aina hiyo ili kukwepa adhabu nyingine katika mechi zijazo

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Ahmed amesema kikosi kilirejea kambini jana baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Fountain Gate ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0

"Tunafahamu ya kwamba tuna mechi ya Ligi ya Mabingwa siku ya Jumapili kwenye dimba la Mkapa kuanzia saa 10 jioni na tayari wageni wetu Gaborone United wamewasili alfajiri ya leo. Mambo yote yamekwenda vizuri na watafanya mazoezi leo na kesho."

"Mchezo wetu wa Jumapili utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Niger na sasa wapo njiani. Kikosi kiliingia kambini jana baada ya mchezo dhidi ya Fountain Gate walirudi kambini na wapo timamu, hakuna mtu yeyote ambaye alipata majeraha. Watakaokosa mchezo ni Mohammed Bajaber na Abdulrazak Hamza."

"Nipo hapa kuwathibitishia kwamba mechi yetu ya Jumapili haitakuwa na mashabiki kutumikia adhabu ya CAF. Kilichosababisha ni mchezo ni dhidi ya Al Masry, kuna shabiki aliingia uwanjani na kuna mashabiki waliwasha moto."

"Adhabu hiyo inakwenda pamoja na faini ya Dola 50,000 kama Tsh. 120 milioni hivi. Niwaase mashabiki wenzangu wa Simba, uache vitendo vya vurugu uwanjani. Kwanza tuanze ulinzi wa wenyewe kwa wenyewe ukiona mtu anataka kuwasha zile fire works mzuie, ukiona mtu anataka kuingia uwanjani tushirikiane kumzuia ikiwezekana kumtoa uwanjani. Angalia mechi kama hii tunakwenda uwanjani bila mashabiki. Hatupo hapa kulaumiana ila kukumbushana,” alisema Ahmed

Katika hatua nyingine, klabu ya Simba imeandaa utaratibu kwa mashabiki wa jijini Dar es salaam kushuhudia mchezo huo pamoja katika viwanja vya Mwembeyanga

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
6h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
10h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
11h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
13h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
16h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
16h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
16h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
18h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
22h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’