Local,Normal News,Yanga

Kocha Yanga amtetea Dube

Joel JJ By Joel JJ
β€’
26 Sep 2025
Kocha Yanga amtetea Dube

Kocha Mkuu wa Yanga Romain Folz amesema ana imani na mshambuliaji Prince Dube licha ya kukosa nafasi nyingi katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Wiliete SC

Kesho Jumamosi Yanga itakuwa mwenyeji wa Wiliete SC katika uwanja wa Benjamin Mkapa ikiwa kifua mbele kufuatia ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Angola

Dube alikuwa miongoni mwa wafungaji katika mchezo huo ambao Aziz Andabwile na Edmund John pia walifunga mabao. Dube pia alipoteza nafasi kadhaa za wazi na kuibua mijadala katika mitandao ya kijamii

Folz amesema ana imani na mshambuliaji huyo raia wa Zimbabwe na ndio maana aliendelea kumuacha dimbani katika mchezo huo na hatimaye akafunga

Folz raia wa Ufaransa amesema jambo muhimu kwa timu yake kwa sasa ni kuwa wanatengeneza nafasi nyingi ingawa bado ufanisi wao sio mzuri sana na hivyo ataendelea kufanyia kazi mapungufu hayo katika uwanja wa mazoezi

"Bado hatuko katika changamoto kubwa ingawa ni kweli ufanisi wetu katika matumizi ya nafasi hauridhishi, tutaendelea kufanya kazi katika uwanja wa mazoezi ili tuboreshe"

"Lakini lazima niwaamini wachezaji wangu pale ninapowapa majukumu. Mfano Prince Dube alipoteza baadhi ya nafasi za wazi katika mchezo uliopita Angola, niliendelea kumuacha uwanjani kwa sababu namuamini"

"Na imani hiyo ilileta matunda kwani aliweza kufunga baadae, Sasa kama ningemtoa labda dakika ya 60 pengine mambo yangeweza kuwa tofauti"

"Tunatengeneza nafasi nyingi ni kweli, lakini pia tunafunga mabao kupitia nafasi hizo, tutaendelea kufanya kazi kwenye uwanja wa mazoezi ili tuongeze ufanisi zaidi mbele ya lango," alisema Folz

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’