Baada ya kuruhusu mabao matano katika mechi mbili za kirafiki, mkufunzi wa Simba Dimitar Pentev ameweka wazi mpango mkakati wake wa kuboresha eneo la ulinzi
Simba licheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Al Hilal ambapo mechi ya kwanza iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 na mechi ya pili wekundu hao wa Msimbazi wakakubali kupoteza kwa mabao 4-1
Katika mazoezi yanayoendelea Mo Simba Arena, Pentev ameoneka kuweka mkazo na kutoa maelekezo mengi vile anataka wachezaji wacheze pale timu inapokuwa haina mpira
Kocha huyo raia wa Bulgaria anapendelea mfumo wa 4-3-3 huku akiwataka wachezaji wake kucheza pamoja wakiwa na mpira na hata bila mpira 'tatal football'
Pentev amesema mechi dhidi ya Al Hilal zimempa mwanga wa nini anapaswa kuboresha na pia wachezaji gani wanaweza kuendana na mbinu zake
"Tunahitaji kuwa na timu inayocheza kwa mpangilio, inayoshambulia kwa hesabu na kujilinda kwa pamoja, mechi hizi zimeniwezesha kuona nani yuko tayari kupigania nembo ya Simba, nadhani kila kitu kitakaa sawa, " alisema Pentev
Simba inakamilisha maandalizi yake leo kabla ya kusafiri kuelekea Eswatin siku ya kesho Alhamisi kuikabili Nsingizini Hotspurs kuwania tiketi ya kufuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika
Mechi ya mkondo wa kwanza itapigwa Jumapili Oktoba 19 na marudiano kupigwa wiki moja baadae jijini Dar es salaam