Jumamosi Oktoba 18 katika uwanja wa Bingu, Yanga itakuwa ugenini kuikabili Silver Strikers katika mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika
Habari njema ni kuwa Wananchi wana uhakika wa sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wao kwani licha ya wale wanaoishi nchini Malawi, kuna msafara utaondoka leo kuelekea Malawi kuongeza hamasa katika mchezo huo
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema zaidi ya mabasi 40 yataondoka leo kulekea Malawi
"Msafara wa wanachama na mashabiki utaondoka Jumatano (leo) ambapo mpaka sasa tuna uthibitisho wa zaidi ya mabasi 40 kuelekea Malawi"
"Viongozi na wachezaji wao wataondoka siku ya Alhamisi ambapo timu ikifika Malawi tutakuwa na 'session' mbili au tatu za mazoezi kuelekea siku ya mchezo ambayo ni Jumamosi," alisema Kamwe
Yanga imepania kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa kwa msimu wa tatu mfululizo. Wananchi wanahitaji kuanza vyema ugenini kabla ya mechi ya pili itakayopigwa jijini Dar es salaam Oktoba 25