Kiungo mshambuliaji wa Simba Mohammed Bajaber amepona majeraha yaliyomuweka nje tangu mwezi Julai wakati wa pre-season nchini Misri
Meneja wa habari na mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amefichua kuwa Bajaber ameendelea na program maalum kuimarisha utimamu wa mwili kabla ya kuanza rasmi kuonekana kwenye kikosi cha kwanza
Baada ya kumsubiri kwa muda mrefu, hatimaye ni suala la muda kwa mashabiki wa Simba kumshuhudia nyota huyo raia wa Kenya













