Muda mchache baada ya Singida Black Stars kukubali kumwachia Clatous Chama atimkie Simba, uongozi wa klabu hiyo upo kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili wa kiungo Mkongomani, Linda Mtange kutoka Aigles Du Congo.
Chama aliitumikia Singida Black Stars kwa miezi sita akitua mwanzoni mwa msimu huu akitokea Yanga na alihudumu kwa msimu mmoja akitokea Simba.
Chanzo cha kuaminika kutoka Singida Black Stars, kimebainisha kuwa wamemuachia Chama baada ya kupata mbadala sahihi ambaye ataweza kuipa vitu vingi zaidi ndani ya timu yao.
βNi kweli Chama ameondoka Singida Black Stars na tayari tumeshampata mbadala wake ambaye tunaamini ataweza kufanya mambo makubwa ndani ya timu, makubaliano ya kumalizana na kiungo huyo yapo katika hatua za mwisho," kilieleza chanzo
Pamoja na Chama, Singida BS imewapoteza wachezaji wengine Nickson Kibabage ambaye pia kajiunga na Simba, Mohamed Damaro aliyejiunga na Yanga na Idris Diomande aliyetua Azam Fc