Simba kufanya maajabu Tunisia?

Joel JJ By Joel JJ • 21st January 2026


Simba kufanya maajabu Tunisia?

Kikosi cha Simba kiliondoka jijini Dar es salaam mapema leo kuelekea Tunisia tayari kwa mchezo wa raundi ya tatu kundi D ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL).

Simba imeelekea Tunisia ikitambua hatma ya kufuzu hatua ya robo fainali iko mikononi mwa mechi mbili zinazofuatana dhidi ya Esperance.

Ikiwa imeshindwa kuokota alama katika mechi zilizopita, Mnyama hapaswi kupoteza mchezo huko Tunisia na ni lazima ahakikishe anashinda mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki ijayo jijini Dar es salaam.

Simba ilikutana na mazingira kama haya mwaka 2023 kwenye michuano hiyo ya ligi ya mabingwa ambapo ilipoteza mechi mbili za kwanza lakini ilifanikiwa kufuzu hatua robo fainali baada ya kushinda mechi tatu kati ya nne zilizosalia.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali anaamini Wekundu hao wa Msimbazi wana nafasi ya kurejea kile walichofanya mwaka 2023 na kazi hiyo wanakwenda kuianza huko Tunisia.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Ahmed ameandika ujumbe huu;

"Mwaka 2023 Mnyama kapoteza mechi mbili za makundi ligi ya mabingwa Afrika, dhidi ya Horoya na Raja Casablanca

Mechi ya tatu dhidi ya Vipers, Wana Simba tukaianza safari ya kilometa zaidi 1600 kutoka Dsm hadi Jinja Uganda mwendo wa saa 49 kwenda kuipigania Simba yetu

Hatukukaa kinyonge kisa tumepoteza mechi mbili na hatukukata tamaa bali tukaingia vitani kuipambania Simba yetu

Katikati ya vita hautakiwi kutia huruma wala kuleta unyonge kwani machozi hayamtishi mpinzani

Vita ikiwa ngumu hautafuti sababu ya kuikimbia bali ni kuongeza nguvu ya kupambana

Tunakwenda Tunisia kwa spirit kama tuliyoenda nayo Uganda, kurejesha matumaini ya Mnyama kwenye ligi ya Mabingwa

Unadhani ni ngumu?? Unadhani haiwezekani hakuna lisilowezekana kwa Simba Sports lnsha Allah

Let’s go Wana Simba tuwaunge mkono Wachezaji wetu, tuwape comfortability ya kufanya kazi na kubwa zaidi tuwaombee," aliandika Ahmed


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.