Baada ya kutua mji wa Alexandria ambako mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly utapigwa, kikosi cha Yanga jioni kimefanya program yake ya kwanza ya mazoezi.
Wananchi watakamilisha maandalizi yao ya mwisho katika uwanja wa Borg El Arab siku ya kesho, mchezo ukitarajiwa kupigwa katika uwanja huo.






