Singida BS yashusha kiungo kutoka Burundi

Joel JJ By Joel JJ β€’ 22nd January 2026


Singida BS yashusha kiungo kutoka Burundi

Baada ya kuachana na Clatous Chama aliyetimkia Simba, klabu ya Singida Black Stars imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Mossi Nduwume.

Nduweme anatua Singida BS akitokea klabu ya Flambeau CFC ya ligi kuu ya Burundi.

Nyota anatajwa kusaini mkataba wa miaka mitatu na walima alizeti hao.

Anatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa, Januari 23 kuanza majukumu yake na Singida BS ambayo kwa sasa iko visiwani Zanzibar tayari kwa mchezo dhidi ya Otoho michuano ya kombe la Shirikisho siku ya Jumapili.

Nduwume tayari ameshaagwa na Flambeau CFC


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.