Manchester United imetangaza kuwa kiungo wao Casemiro ataondoka klabuni hapo mara baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 alijiunga na Manchester United akitokea Real Madrid mwaka 2022 kwa ada ya pauni milioni 70, na amefanikiwa kucheza jumla ya mechi 146.
Alifunga bao la kwanza katika ushindi wa fainali ya Kombe la Carabao mwaka 2023 dhidi ya Newcastle, huku Manchester United wakimaliza katika nafasi ya tatu ya Ligi Kuu ya England msimu wake wa kwanza.
Hata hivyo, mwaka jana alitajwa na mmiliki mwenza mpya wa klabu hiyo, Sir Jim Ratcliffe, ambaye aliambia BBC Sport kuwa baadhi ya wachezaji hawana ubora wa kutosha na wanalipwa mishahara mikubwa kupita kiasi.
Casemiro amesema ataendelea kuwa mfuasi wa Manchester United wakato wote
βNitaitunza Manchester United moyoni mwangu maisha yangu yote. Huu si wakati wa kuaga; bado kuna kumbukumbu nyingi za kuunda katika miezi minne ijayo. Bado tuna mambo mengi ya kupigania pamoja; umakini wangu wote, kama ilivyo kawaida, utaendelea kuwa katika kutoa kila nilicho nacho ili kusaidia klabu yetu kufanikiwa,β alisema