International,Normal News,Manchester United, Real Madrid

Casemiro na Manchester United mwisho umewadia

Joel JJ By Joel JJ
β€’
23 Jan 2026
Casemiro na Manchester United mwisho umewadia

Manchester United imetangaza kuwa kiungo wao Casemiro ataondoka klabuni hapo mara baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 alijiunga na Manchester United akitokea Real Madrid mwaka 2022 kwa ada ya pauni milioni 70, na amefanikiwa kucheza jumla ya mechi 146.

Alifunga bao la kwanza katika ushindi wa fainali ya Kombe la Carabao mwaka 2023 dhidi ya Newcastle, huku Manchester United wakimaliza katika nafasi ya tatu ya Ligi Kuu ya England msimu wake wa kwanza.

Hata hivyo, mwaka jana alitajwa na mmiliki mwenza mpya wa klabu hiyo, Sir Jim Ratcliffe, ambaye aliambia BBC Sport kuwa baadhi ya wachezaji hawana ubora wa kutosha na wanalipwa mishahara mikubwa kupita kiasi.

Casemiro amesema ataendelea kuwa mfuasi wa Manchester United wakato wote

β€œNitaitunza Manchester United moyoni mwangu maisha yangu yote. Huu si wakati wa kuaga; bado kuna kumbukumbu nyingi za kuunda katika miezi minne ijayo. Bado tuna mambo mengi ya kupigania pamoja; umakini wangu wote, kama ilivyo kawaida, utaendelea kuwa katika kutoa kila nilicho nacho ili kusaidia klabu yetu kufanikiwa,” alisema

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
49m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’