Local,Transfer News,Yanga,Kabylie

Ecua aibukia JS Kabylie

Joel JJ By Joel JJ
β€’
27 Jan 2026
Ecua aibukia JS Kabylie

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Young Africans SC, Celestin Ecua, amekamilisha rasmi uhamisho wake wa mkopo kwenda klabu ya JS Kabylie ya Algeria, katika hatua inayohitimisha safari yake ya muda mfupi ndani ya kikosi cha Wananchi.

Ecua ametua Algeria kwa mkopo wa mwaka mmoja, baada ya Yanga kufanya maamuzi ya kumwondoa kwenye mipango ya kikosi cha msimu huu, huku klabu ikichagua kufanya maboresho makubwa kupitia dirisha dogo la usajili.

Awali, nyota huyo alikuwa akihusishwa na uhamisho kwenda Sekhukhune United ya Afrika Kusini, sambamba na kiungo mwingine Mohamed Doumbia, ambaye naye pia hakuwa sehemu ya mipango ya kocha wa Yanga.

Hata hivyo, JS Kabylie imeibuka kuwa kituo kipya cha Ecua, ikimpa nafasi ya kuendeleza kipaji chake kwenye moja ya ligi zenye ushindani mkubwa barani Afrika.

Hatua ya Yanga kumuacha Ecua inakuja baada ya klabu hiyo kuongeza nguvu mpya kupitia usajili wa wachezaji watatu wa kigeni kwenye dirisha dogo, ambao ni Depu, Allan Okello na Yao Kouassi. Sambamba na hilo, Wananchi wameamua kuachana na baadhi ya wachezaji wa kigeni akiwemo And Boyeli, Mohamed Doumbia na sasa Celestin Ecua.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
2h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
5h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
7h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
9h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
11h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
12h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
17h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’