Local,Normal News,Simba

Kiungo Kutoka Cameroon Atua Dar Kujiunga na Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
27 Jan 2026
Kiungo Kutoka Cameroon Atua Dar Kujiunga na Simba

Klabu ya Simba SC imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kuimarisha kikosi chake kwa kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Inno Jospin Loemba (21) kutoka klabu ya Colombe Sports ya Cameroon.

Loemba tayari ametua jijini Dar es Salaam, hatua inayofungua ukurasa mpya katika safari yake ya soka barani Afrika Mashariki.

Taarifa kutoka ndani ya klabu zinaeleza kuwa huenda utambulisho wake ukafanyika leo, kabla ya kujiunga moja kwa moja na kikosi cha Simba kinachorejea mazoezini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mashujaa FC, unaotarajiwa kuchezwa siku ya Alhamisi.

Usajili wa Loemba unakuja katika kipindi muhimu kwa Simba, ambayo ina ratiba ngumu ya michezo. Baada ya pambano dhidi ya Mashujaa FC, wekundu wa Msimbazi wanatarajiwa kurejea mawindoni kimataifa, wakiweka nguvu zao kwenye mchezo mkubwa dhidi ya Esperance de Tunis, utakaopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumapili.

Licha ya kusajiliwa kutoka klabu ya Cameroon, Loemba ni raia wa Congo Brazzaville, na amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa Colombe Sports, ambapo aliwahi pia kuwa nahodha wa kikosi hicho ishara ya uwezo wake wa uongozi na uzoefu uwanjani licha ya umri wake mdogo.

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
36m ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
49m ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
4h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
8h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
9h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
10h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
11h ago
READ MORE β†’