International,Normal News,Real Madrid, Liverpool, Manchester City

Trent mambo magumu Real Madrid, kurudi Uingereza?

Joel JJ By Joel JJ
β€’
27 Jan 2026
Trent mambo magumu Real Madrid, kurudi Uingereza?

Hatma ya beki wa kulia wa Real Madrid na timu ya taifa ya England, Trent Alexander-Arnold (27), inaendelea kuwa gumzo barani Ulaya, huku nyota huyo akiripotiwa kukumbana na changamoto kubwa ndani ya kikosi cha Los Blancos tangu kuanza kwa dirisha la usajili la majira haya ya kiangazi.

Taarifa zinaeleza kuwa Manchester City inaendelea kumfuatilia kwa karibu Trent, ikivutiwa zaidi na uwezo wake wa kupandisha mashambulizi, kutoa pasi za mwisho na kusoma mchezo kwa haraka. Mabingwa hao wa England wanaamini kuwa wanaweza kuipata saini yake iwapo watawasilisha ofa nono kwa Real Madrid.

Trent amekuwa akihusishwa na nia ya kuondoka BernabΓ©u, kufuatia kushindwa kujihakikishia nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza. Licha ya kurejea uwanjani baada ya kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara, kiwango chake kimeelezwa kutokuwa cha kuridhisha kwa benchi la ufundi la Madrid, hali inayozua maswali kuhusu mustakabali wake.

Inaelezwa kuwa uongozi wa Real Madrid haujamfunga Trent milango ya kutoka, na uko tayari kusikiliza ofa kutoka kwa klabu zitakazovutiwa na huduma yake. Baadhi ya mabosi wa klabu hiyo wanaamini kuwa mchezaji huyo hajaendana kikamilifu na falsafa ya timu, jambo linaloweza kuharakisha uamuzi wa kumuacha endapo ofa sahihi itawasilishwa.

Kwa upande wa Manchester City, nia ya kumsajili Trent inachangiwa na idadi kubwa ya majeruhi katika safu ya ulinzi, hali iliyomfanya kocha wao kuangalia chaguo mbadala lenye uzoefu wa juu katika soka la Ulaya.

Hadi sasa, Real Madrid bado haijatoa msimamo rasmi kuhusu mustakabali wa beki huyo wa zamani wa Liverpool, lakini dalili zinaonyesha kuwa milango ipo wazi kwa mazungumzo.Β 

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’