Yanga imerejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC baada ya kuichapa Dodoma Jiji mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex.
Wananchi walilazimika kutokea nyuma kupata ushindi huo muhimu baada ya Dodoma Jiji kufunga bao la kutangulia kupitia William Edgar dakika ya 41.
Hata hivyo Yanga ilisawazisha bao hilo dakika ya 45 kupitia mkwaju wa penati uliowekwa kambani na Depu baada ya Frank Assink kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari.
Kipindi cha pili Yanga iliongeza kasi ya mashambulizi hasa baada kuingia kwa Duke Abuya, Allan Okello na Mohamed Damaro.
Wananchi waliongeza mabao mawili kupitia kwa Depu aliyefunga bao lake la tatu ndani ya mechi mbili kupitia mpira wa kichwa kabla ya Prince Dube kuongeza uongozi zaidi akitumia makosa ya safu ya ulinzi ya Dodoma Jiji ambao walipoteza mpira langoni kwao wakati wakijenga shambulizi kutokea nyuma.
Depu ameibuka nyota wa mchezo huo baada ya kufunga mabao mawili, pengine angeweza kuondoka na mpira kama angeongeza umakini.
Yanga imefikisha alama 22 na kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kucheza mechi nane.