Simba leo imerejesha furaha ya mashabiki wake ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mashujaa Fc katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Isamuhyo, Mbweni jijini Dar es salaam.
Mabao ya Libasse Gueye na Suleiman Mwalimu yalitosha kuihakikisha Simba alama tatu muhimu katika mchezo ambao Simba ilicheza kwa mamlaka zaidi huku nyata wapya hasa Anicet Oura na Gueye wakidhihirisha ubora wao.
Pengine Simba ilistahili kupata ushindi mnono zaidi kama matumizi ya nafasi yangekuwa sahihi zaidi huku Kubu Denis akipoteza nafasi adimu ya mkwaju wa penati.
Simba ilizihitaji alama tatu leo ili kurejesha morali ya timu kuelekea mechi ngumu ya ligi ya mabingwa dhidi ya Esperance itakayopigwa Jumapili.
Mnyama sasa anarudi mazoezini kukamilisha maandalizi ya kuikabili Esperance katika mchezo ambao Simba LAZIMA ishinde ili kuweka hai matumaini ya kuisaka tiketi ya robo fainali.



