Dodoma Jiji yamnasa Maguri

Joel JJ By Joel JJ
β€’
30 Jan 2026
Dodoma Jiji yamnasa Maguri

Klabu ya Dodoma Jiji FC imekamilisha usajili wa mshambuliaji mkongwe Elias Maguli (34), hatua inayolenga kuimarisha safu ya ushambuliaji wa timu hiyo kuelekea michezo ijayo ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Maguli ni jina linalofahamika vyema kwenye soka la Tanzania kutokana na uzoefu wake mkubwa na uwezo wa kufumania nyavu. Ndani ya nchi, mshambuliaji huyo amewahi kuzitumikia klabu kadhaa zenye ushindani mkubwa zikiwemo Simba SC, Ruvu Shooting, KMC FC, Geita Gold, Stand United pamoja na Tanzania Prisons, ambako alionyesha kiwango kizuri na kuacha alama katika nyakati tofauti za taaluma yake.

Mbali na uzoefu wa ndani, Maguli pia ana historia ya kucheza soka la kimataifa baada ya kuvitumikia vilabu vya nje ya Tanzania. Ameshacheza katika klabu ya FC Platinum (Zimbabwe), Nakambala (Zambia), AS Kigali (Rwanda) pamoja na Dhofar Club ya Oman, safari iliyomjengea uzoefu mkubwa wa michezo ya ushindani wa juu.

Usajili wa Maguli unaonekana kuwa sehemu ya mkakati wa Dodoma Jiji kuongeza ushindani kikosini, hasa katika eneo la ushambuliaji, kwa kutumia mchanganyiko wa uzoefu na vijana. Uwepo wake unatarajiwa kusaidia sio tu kwenye kufunga mabao, bali pia kuwapa mwanga na mwelekeo washambuliaji chipukizi waliopo ndani ya kikosi.

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
1h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
3h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
4h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
5h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
6h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
7h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
7h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
20h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’