Mchezo wa nne kundi B ligi ya mabingwa barani Afrika kati ya Yanga dhidi ya Al Ahly umemalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1.
Mchezo huo uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex ulishuhudia Yanga ikitangulia kufunga dakika ya 45 kupitia Ibrahim Bacca baada ya piga nikupe langoni mwa Al Ahly kufuatia krosi ya Pacome Zouzoua kutoka upande wa kulia.





