Local,Normal News,Yanga, Ahly

Yanga, Al Ahly hakuna mbabe New Amaan Complex

Joel JJ By Joel JJ
β€’
31 Jan 2026
Yanga, Al Ahly hakuna mbabe New Amaan Complex

Mchezo wa nne kundi B ligi ya mabingwa barani Afrika kati ya Yanga dhidi ya Al Ahly umemalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1.

Mchezo huo uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex ulishuhudia Yanga ikitangulia kufunga dakika ya 45 kupitia Ibrahim Bacca baada ya piga nikupe langoni mwa Al Ahly kufuatia krosi ya Pacome Zouzoua kutoka upande wa kulia.

Yanga ilikuwa bora kwa muda mwingi wa mchezo hasa kipindi cha kwanza wakitengeneza nafasi nyingi kuliko wapinzani wao lakini hawakuweza kuzitumia.

Kipindi cha pili ni Al Ahly waliorejea na kasi kubwa wakisaka bao la kusawazisha huku Yanga wakiendelea kushambulia kwa kushitukiza.

Aliou Dieng ndiye aliyeisawazishia Al Ahly baada ya mpira wa kona ambao walinzi wa Yanga walizembea kuondoa.

Yanga ilipata nafasi adimu kwenye kipindi cha pili lakini Maxi Nzengeli hakuweza kuitumia huku Duke Abuya na Prince Dube wakipoteza nafasi pia.

Ni matokeo ambayo unaweza kusema yataziacha timu zote zikiridhika kwani ulikuwa mchezo ambao kila kitu ilitengeneza nafasi na pengine kushinda.

Yanga imefikisha alama tano ikiendelea kusalia nafasi ya pili kundi B huku Al Ahly wakiongoza na alama zao nane.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
45m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’