Local,Normal News,Simba

Ahmed awatuliza mashabiki baada ya Simba kukwama ligi ya mabingwa

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1 Feb 2026
Ahmed awatuliza mashabiki baada ya Simba kukwama ligi ya mabingwa

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amewapa pole Wanasimba wote baada timu yao kushindwa kufuzu robo fainali ya ligi ya mabingwa leo wakilazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Esperance.

Ahmed amesema ni msimu mbaya kwa Simba kushindwa kufuzu robo fainali baada ya kufanya hivyo kwa takribani misimu saba mfululizo.

Ahmed amesema kwa sasa Simba inaelekeza nguvu zake kwenye mechi mbili zilizobaki kukamilisha ratiba na kuwekeza nguvu kubwa zaidi kwenye mashindano ya ndani.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Ahmed ameandika ujumbe huu.

"Umekua msimu mbaya kwetu kwenye michuano ya kimataifa, inauma lakin hatuna budi kukubali kuwa msimu huu umekua mgumu kwetu

Kama ambavyo misimu mingine tunafuzu kwenda Robo Fainali na wengine wanashindwa basi msimu imekua zamu yetu kuanguka

Hatuna sababu ya kuvurugana wala kutafuta mchawi itoshe kusema msimu huu haukuwa wetu au haikua rizki yetu

Tumalizie mechi mbili zilizobaki baada ya hapo tuwekeze nguvu kwenye mashindano ya ndani huku bado tuna nafasi kubwa ya kufanya vizuri

Poleni ndugu zangu Wana Simba, Tulichozea kufanya tumeshindwa kufanya safari hii, Tukubali kuwa huu ni msimu mbaya kwetu na hutokea kwa timu yeyote Duniani

Asanteni na poleni wale wote waliotoa nguvu zao kuipambania Simba ishinde hii leo, Asanteni wale wote waliokuja Uwanjani hii leo, Tanatambua na kuthamini mchango wenu kwenye kuipambania Simba yetu

Itoshe kusema Asante Mungu wewe ndio mpangaji wa yote

Hadi wakati mwingine Wanyama, Hakuna kukataa tamaa maisha ya mpira bado yanaendelea"

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’