Local,Normal News,Simba

Kocha Simba awapa tumaini mashabiki

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Feb 2026
Kocha Simba awapa tumaini mashabiki

Kocha Mkuu wa Simba Steve Barker amewataka Wanasimba kuendelea kuwa wamoja huku akiahidi kikosi chake kupambana ili wamalize michuano ya ligi ya mabingwa kwa heshima na zaidi kufanya vyema katika mashindano mengine.

Juzi Barker alishuhudia kikosi chake kikipoteza uongozi wa mabao mawili kipindi cha kwanza na kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Esperance ya Tunisia matokeo ambayo yamefuta matumaini ya Simba kufuzu robo fainali.

Barker amesema walikuwa na mkakati mzuri walioukamilisha kwa usahihi katika kipindi cha kwanza lakini kukosekana kwa umakini na presha ya mchezo ikawagharimu kwenye lipindi cha pili na kuruhusu mabao mawili.

"Kufungwa mabao mawili na kushindwa kushinda kutoka kwenye nafasi tuliyokuwa nayo ni jambo linaloumiza, hasa kwa sababu wachezaji walifanya kazi kubwa sana kipindi cha kwanza"

"Tutaendelea kufanya kazi kwa bidii, kupambana kwa ajili ya beji ya Simba na kuhakikisha timu inaendelea kukua na kuwa bora zaidi, natambua hali ambayo mashabiki wetu wanajisikia, lakini hiki ni kipindi cha mpito na niwahakikishie kuna nyakati nzuri za furaha zinakuja ni suala la muda tu,” alisema Barker.

Kwa sasa Simba imesaliwa na mechi mbili katika hatua ya makundi kwa kucheza ugenini dhidi ya Petro Atletico huko Angola kabla ya kufunga pazia katika michuano hiyo kimataifa kwa kucheza dhidi ya vinara Stade Malien.

Mchezo dhidi ya Petro Atletico unatarajiwa kupigwa Jumamosi, Februari 07 huko Angola na kisha Simba kurejea Dar kumalizana na Stade Malien Februari 14

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
7h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
11h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
12h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
14h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
16h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
17h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
17h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
19h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
23h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’