Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kufungulia uwanja wa KMC Complex baada ya kufanyiwa maboresho.
Uwanja huo ulifungiwa kutokana na miundombinu yake kutofaa kutumika kwa mujibu wa kanuni kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya kanuni ya leseni za klabu.




