Local,Normal News,Yanga

Mzize bado kidogo Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
5 Feb 2026
Mzize bado kidogo Yanga

Mshambuliaji Clment Mzize ni miongoni mwa wachezaji waliosafiri na kikosi cha Yanga Morocco kuelekea mchezo dhidi ya AS FAR, raundi ya tano, kundi B ligi ya mabingwa barani Afrika.

Mzize ameendelea kuimarika baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu unaweza kusema ni suala la muda tu kwake kuonekana uwanjni.

Pengine mshambuliaji huyo ambaye aliongeza mkataba wa kuendelea kusalia Yanga kwenye dirisha la Julai licha ya timu nyingi kumuhitaji, anaweza kuwa tayari kurejea kwenye mchezo dhidi ya JS Kabylie utakaopigwa Februari 14

Mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves ameweka wazi kuwa hana mpango wa kumtumia Mzize katika mchezo dhidi ya AS FAR kwa kutambua umuhimu wa kumlinda na kuhakikisha harudi tena kwenye majeraha kama ilivyotokea huko nyuma

"Ni jambo jema kwetu kuona Clement (Mzize) anafanya mazoezi kikamilifu na timu, hatutakuwa na haraka kumtumia katika mechi hizi zenye presha kubwa kwani afya ya mchezaji ni kipaumbele kikubwa kuliko presha ya matokeo ya muda mfupi.," alisema

Jumamosi Yanga itakuwa ikisaka ushindi au angalau sare kwenye mchezo dhidi ya AS FAR ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
7h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
11h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
12h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
14h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
16h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
17h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
17h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
19h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
23h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’