Local,Normal News,Simba, Malien, Esperance

Stade Malien ilivyozima Esperance, Simba kundi D

Joel JJ By Joel JJ
β€’
9 Feb 2026
Stade Malien ilivyozima Esperance, Simba kundi D

Stade Malien imekuwa timu ya kwanza kukata tiketi ya robo fainali michuano ya ligi ya mabingwa kutoka kundi D baada ya kuichapa Esprance bao 1-0 hapo jana.

Baada ya ushindi huo, Stade Malien walifikisha alama 11 na kujihakikisha kuongoza kundi D, kwani hakuna timu nyingine inaweza kufikisha alama hizo katika kundi.

Esperance na Petro Atletico kila moja ina alama sita mechi ya mwisho baina yao itaamua timu ya kutinga robo fainali sambamba na Stade Malien.

Kilichofanywa na Stade Malien hakikutarajiwa kwani baada ya droo ya makundi ni Simba na Esperance zilizokuwa zikipewa nafasi ya kuvuka katika kundi hilo.

Katika ranking za CAF Esperance wako nafasi ya tatu huku Simba wakiwa nafasi ya tano Stade Malien hawamo hata kwenye 20 bora lakini msimu huu wamewashangaza wengi, ikiwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo kundi D.

Unaweza kusema wamenufaika kwa kuporomoka kiwango kwa klabu za Simba na Esperance lakini pia wana kikosi bora.

Malien wanaweza kufanya vyemaΒ  hatua inayofuata na pengine hata kufika nusu fainali kama wataendeleza kiwango chao cha sasa.

Mechi ya mwisho kundi D watasafiri Dar es salaam kuumana na Simba katika mchezo utakaopigwa Februari 14 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kwa Simba huu utakuwa mchezo wa kisasi baada ya kupoteza mchezo wa kwanza timu hizo zilipokutana Mali ingawa matokeo yake hayatakuwa na athari yoyote kwenye msimamo wa kundi.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
3h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
5h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
6h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
6h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’