William Edgar, Goncalves washinda tuzo za ligi kuu Januari

Joel JJ By Joel JJ β€’ 9th February 2026


William Edgar, Goncalves washinda tuzo za ligi kuu Januari

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves ameshinda tuzo ya kocha bora wa ligi kuu ya NBC kwa mwezi Januari 2026.

Goncalves ametwaa tuzo hiyo akiwashinda Juma Mgunda wa Namungo Fc na Yusuph Chipo wa Mtibwa Sugar.

Aliingoza Yanga kushinda mechi zilizopigwa Januari, dhidi ya Mashujaa Fc (6-0) na dhidi ya Dodoma Jiji (3-1).

Aidha tuzo ya mchezaji bora imechukuliwa na William Edgar wa Dodoma Jiji ambaye amewashinda Laurindo Aurelio (Yanga) na Fabrice Ngoy wa Namungo Fc.

Aidha Kamati ya tuzo ya TFF imeteua mabao matatu yaliyofungwa Januari kuwania tuzo ya goli bora la mwzi.

  1. Laurindo Aurelio - (Yanga dhidi ya Dodoma Jiji)
  2. Libasse Gueye (Simba dhidi ya Mashujaa)
  3. Lassa Kialla (Coastal Union dhidi ya KMC)

Mashabiki wanaweza kupiga kura kupitia kurasa rasmi za mtandao wa Instagram @ligikuu, @tanfootball na #nbc_tanzania


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.