International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Februari 12 2026

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Feb 2026
Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Februari 12 2026

Bayern Munich wanapanga kumsajili kipa wa Brighton, Bart Verbruggen (23), katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (Talksport)

Chelsea wako tayari kupambana na Bayern Munich kwa ajili ya Verbruggen na wako tayari kutoa pauni milioni 50 inayotakiwa na Brighton kwa ajili ya kipa huyo wa kimataifa wa Uholanzi. (Teamtalk)

Beki wa England wa Manchester City, John Stones (31), huenda akaondoka klabuni hapo majira ya kiangazi mkataba wake utakapomalizika, huku Bayern Munich wakionyesha nia ya kumsajili. (Caught Offside) Atletico Madrid wanachunguza uwezekano wa kumsajili beki wa Chelsea na Hispania, Marc Cucurella (27). (Fichajes)

Aston Villa wanamwania kiungo wa England wa Nottingham Forest, Morgan Gibbs-White (26), lakini Forest wanaweza kutaka ada nono ya hadi pauni milioni 65. (TeamTalk)

Tottenham wanamuona beki wa Real Madrid na Ujerumani, Antonio Rudiger (32), kama mbadala wa Cristian Romero (27) iwapo beki huyo wa Argentina ataondoka na kujiunga na Real Madrid. (Fichajes)

Borussia Dortmund wanataka kumpa beki wa Ujerumani Nico Schlotterbeck (26) mkataba mpya, huku Real Madrid wakionyesha nia ya kumsajili. (Bild)

Aliyekuwa kocha wa Marseille, Roberto de Zerbi, anaweza kuwa tayari kuinoa Tottenham, licha ya awali kupendelea kusubiri nafasi ya kuifundisha Manchester United. (TeamTalk)

Nottingham Forest watajaribu tena kumsajili kiungo wa Celtic na Ubelgiji, Arne Engels (22), majira ya kiangazi baada ya kushindwa kumsajili mwezi Januari. (Football Insider)

Juventus na Inter Milan zinatarajiwa kuwania saini ya kipa wa Tottenham na Italia, Guglielmo Vicario (29), majira ya kiangazi. (Gazzetta)

Manchester United wanaonekana kuongoza katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Everton na Senegal, Iliman Ndiaye (25), majira ya kiangazi. (Teamtalk)

Newcastle United huenda wakamgeukia kiungo wa Roma na Italia, Lorenzo Pellegrini (29), iwapo watampoteza Sandro Tonali (25) majira ya kiangazi. (Football Insider)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’