Klabu ya Tanzania Prisons imetoa taarifa kuwa itacheza mechi za ligi kuu uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma wakati uwanja wa Sokoine, Mbeya ukiendelea na ukarabati.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) hivi karibuni lilitangaza kufungia uwanja wa Sokoine baada ya kutokidhi vigezo vya kikanuni.
Februari 22 Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Simba katika mchezo wa ligi kuu ambao sasa utapigwa mkoani Dodoma.
Kabla ya mchezo huo, Februari 19 Tanzania Prisons wanakabiliwa na mchezo wa kombe la CRDB ambao umepangwa kupigwa uwanja wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.




