International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa February 20 2026

Joel JJ By Joel JJ
β€’
20 Feb 2026
Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa February 20 2026

Paris St-Germain imekuwa ikimfuatilia mshambuliaji wa Norway klabu ya Manchester City, Erling Haaland kwa muda mrefu, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 huenda akaelekea Uhispania, ikiamua kuhama. (Team Talk)

Klabu ya Aston Villa inataka kumsajili kiungo wa kati wa Wales Harry Wilson kwa uhamisho wa bure kutoka Fulham msimu huu wa joto, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 pia akidaiwa kunyantiwa na Everton. (Telegraph - usajili unahitajika)

Beki wa Tottenham mwenye umri wa miaka 27 na Argentina Cristian Romero na kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher, 26, ni miongoni mwa wachezaji ambao wanatarajiwa kuondoka Spurs msimu huu wa joto ikiwa ikiwa klabu hiyo itashuka daraja. (Athletic- Usajili unahitajika)

Barcelona na Atletico Madrid zinapigana vikumbo kwa kiungo wa kimataifa wa Ureno Bernardo Silva, ambaye mkataba wake Manchester City unakalika msimu huu wa joto, huku klabu za Juventus na Monaco pia zikimuwania mchezaji huyo wa aliye na umri wa miaka 31. (Teamtalk)

Carlo Ancelotti ananuia kusaini mkataba wa miaka minne kama kocha wa Brazil. (Movistar kupitia AS - kwa Kihispania)

Mfungaji bora wa muda wote wa Ufaransa Olivier Giroud, ambaye sasa ana umri wa miaka 39, yuko kwenye njia panda kuhusiana na mustakabali wake katika klabu ya Lille ya Ufaransa. (L'Equipe - kwa Kifaransa - usajili unahitajika)

Winga wa Newcastle Muingereza Anthony Gordon, 24, anasema hataruhusu uvumi wa uhamisho umuathiri baada ya kuhusishwa na Liverpool na Arsenal. (Sun) Kipa wa Manchester City Muingereza James Trafford, 23, angelipendelea kuhamia klabu ya Aston Villa badala ya Newcastle United msimu huu wa joto. (Football Insider)

LA Galaxy inafuatilia kwa karibu hali ya Philippe Coutinho huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 ambaye sasa ni mchezaji huru baada ya Vasco da Gama kukubali kusitisha mkataba wa kiungo huyo wa zamani wa Brazil. (AS - kwa Kihispania)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
47m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’