International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumapili February 22 2026

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 Feb 2026
Tetesi za usajili Ulaya, Jumapili February 22 2026

Tottenham na Newcastle wana shauku ya kumrudisha kwenye ligi kuu mshambuliaji wa Al-Hilal wa Uruguay mwenye umri wa miaka 26, Darwin Nunez, ambaye zamani alikuwa Liverpool. (Teamtalk)

Tottenham na Aston Villa ni miongoni mwa vilabu vinavyomfuatilia kiungo wa Lyon wa Jamhuri ya Czech mwenye umri wa miaka 25, Pavel Sulc. (Mail)

Beki wa Uingereza Joe Gomez anaonekana kujiandaa kuondoka Liverpool msimu huu wa joto huku AC Milan na Bayern Munich wakipendezwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Caught Offside)

Roma na Juventus wamejiunga na kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa Argentina wa Bournemouth mwenye umri wa miaka 28, Marcos Senesi mwishoni mwa msimu. (Corriere Dello Sport)

Real Madrid wanaongoza kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa Ujerumani wa Borussia Dortmund, Nico Schlotterbeck, lakini Barcelona pia wana hamu ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (AS)

Newcastle wana shauku ya kumsajili beki wa Uhispania mwenye umri wa miaka 23, Hugo Bueno kutoka Wolves msimu huu wa joto. (Football Insider)

Liverpool inaandaa dau la pauni milioni 83 kwa winga wa Newcastle mwenye umri wa miaka 24 wa Uingereza Anthony Gordon ikiwa mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 33, ataondoka klabuni msimu huu wa joto. (Fichajes)

Everton wanatarajiwa kutoa dau la pauni milioni 30 kwa mshambuliaji wa Chelsea mwenye umri wa miaka 23 wa Uingereza Liam Delap msimu huu wa joto. (Teamtalk)

Crystal Palace wanajaribu kumshawishi Gareth Southgate kuchukua nafasi ya Oliver Glasner kwa msingi wa meneja wa muda hadi mwisho wa msimu. (Football Insider)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
45m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’