Droo ya 32 CRDB Cup hii hapa

Joel JJ By Joel JJ β€’ 24th February 2026


Droo ya 32 CRDB Cup hii hapa

Droo ya hatua ya 32 bora kombe la CRDB ilifanyika mapema leo ambapo mechi zote za raundi ya 32 na 16 zilipangwa.

Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Yanga wao wamepangwa kuchuana na Polisi Tanzania katika hatua ya 32 bora ambapo mshindi wa mchezo huo atachuana na mshindi wa mchezo kati ya Tanzania Prisons dhidi ya TMA Stars kwenye hatua ya 16 bora.

Vigogo wengine wa soka nchini Simba wao watachuana na B19 Fc ambao kama watavuka hatua hiyo kwenye 16 bora watakumbana na mshindi wa mchezo kati ya Dodoma Jiji dhidi ya African Sports.

Azam Fc itachuana na Mbeya Kwanza hatua ya 32 bora ambapo kama itavuka hatua hiyo, itachuana na mshindi wa mchezo kati ya Fountain Gate dhidi ya Gunners Fc.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.