Local,Normal News,Azam, Mtibwa

Azam Fc yamoto, yaichapa Mtibwa Sugar 3-0

Joel JJ By Joel JJ
β€’
26 Feb 2026
Azam Fc yamoto, yaichapa Mtibwa Sugar 3-0

Azam Fc imeendeleza ubabe kwenye ligi kuu ya NBC baada ya kuichapa Mtibwa Sugar mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex Jumatano usiku.

Mshambuliaji Mcongomani Jacques Ngita alikuwa shujaa wa Azam Fc katika mchezo huo akifunga mabao mawili.

Feisal Salum 'Fei Toto' ndiye aliyefungua milango ya Mtibwa Sugar kwa goli la mapema kabla yha Ngita kuongeza mengine mawili.

Ni kipigo cha tatu mfululizo kwa Mtibwa Sugar ambao mchezo uliopita pia walifungwa mabao 3-1 na Singida BS.

Azam Fc wamechupa hadi nafasi ya tano kwenye msimmo wa ligi wakifikisha alama 22, alama moja nyuma ya Simba yenye alama 23 nfasi ya tatu.

Simba ililazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Dodoma Jiji mchezo uliopigwa mapema uwanja wa Jamhuri.

JKT Tanzania iliyokubaki kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Yanga inaendele kushikilia nafasi ya pili ikiwa na alama 28 sawa na Yanga ambayo ulishindi wao dhidi ya JKT Tanzania umewapeleka kileleni mwa msimamo wa ligi.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’