Local,Transfer News,Yanga, Ittihad, International

Al Ittihad imelipa mabilioni kuwanasa Aziz Ki, Lorch

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Mar 2026
Al Ittihad imelipa mabilioni kuwanasa Aziz Ki, Lorch

Klabu kongwe ya Libya, Al-Ittihad Club, imekamilisha rasmi malipo ya ada za uhamisho kwa mabingwa wa Morocco, Wydad Athletic Club, kwa ajili ya kuwasajili nyota wawili waliokuwa wakikitumikia kikosi hicho.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, jumla ya dola za Marekani milioni 1.4 (takribani Sh3.9 bilioni) zimelipwa kukamilisha dili hilo. Kati ya fedha hizo, dola 800,000 (Sh2.04 bilioni) zimelipwa kwa ajili ya kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki, huku dola 600,000 (Sh1.53 bilioni) zikihusu uhamisho wa winga wa Afrika Kusini, Thembinkosi Lorch.

Kukamilika kwa miamala hiyo kunahitimisha rasmi mchakato wa usajili wa wachezaji hao ambao tayari wameanza kuitumikia Al-Ittihad katika msimu wa 2025/26.

Aziz Ki, ambaye aliwahi kung’ara katika Ligi Kuu Tanzania Bara kabla ya kujiunga na Wydad, amekabidhiwa jezi namba 22, huku Lorch akikabidhiwa jezi namba 11 katika kikosi hicho cha Tripoli.

Usajili wa nyota hao unaonyesha dhamira ya Al-Ittihad kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya, huku Wydad wakikamilisha mchakato wa uhamisho kwa mafanikio ya kifedha.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
46m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’