International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne, March 03 2026

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Mar 2026
Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne, March 03 2026

Wachezaji wa Tottenham wanakabiliwa na kupunguzwa kwa mishahara kwa lazima ikiwa klabu hiyo itashushwa kutoka Ligi ya Premia hadi katika ligi ya Ubingwa. (The Athletic - Subscription Required).

Inter Milan wanavutiwa na mlinda lango wa Liverpool na Brazil Alisson, 33, huku Juventus pia wakimtaka. (La Repubblica - Subscription Required in Italy).

Manchester United wanamtaka nahodha wa Newcastle Bruno Guimaraes, 28, kuchukua nafasi ya kiungo Casemiro msimu huu wa joto - huku kiungo huyo wa kati wa United mwenye umri wa miaka 34 akimuidhinisha mchezaji mwenzake wa Brazil. (AS).

Beki wa Spurs Micky van de Ven hana nia ya kuongeza mkataba wake na klabu hiyo inayofanya vibaya huku Barcelona na Real Madrid wakimfuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, 24, kwa ajili ya uhamisho wa majira ya joto. (Nipe Sport).

Bayern Munich wataelekeza mawazo yao kwenye kandarasi mpya kwa mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 32, baada ya mlinzi wa Ufaransa Dayot Upamecano, 27, kutia saini mkataba mpya mwezi uliopita. (Fabrizio Romano).

Liverpool, Arsenal na Barcelona zote zinamfuatilia beki wa Inter Milan mwenye umri wa miaka 26 Alessandro Bastoni. (Caughtoffside).

Arsenal wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili Leon Goretzka wa Bayern Munich mkataba wake utakapokamilika msimu huu wa joto huku kiungo huyo wa kati wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 31 akitamani kucheza Ligi ya Premia licha ya kutakiwa na Inter Milan, Juventus na AC Milan. (Christian Falk vianBayern Insider).

Barcelona wako tayari kuilipa Manchester United ada wanayotaka kubadilisha uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji wa England Marcus Rashford kuwa wa kudumu. (Mirror).

Manchester City wanataka kumsajili tena Lukas Nmecha kutoka Borussia Dortmund. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aliachiliwa na City miaka mitano iliyopita bila kucheza Ligi ya Premia lakini anasakwa na Pep Guardiola(Target).

Manchester United wamemuongeza mkufunzi wa Borussia Dortmund Niko Kovac, 54, kwenye orodha yao ya kuteuliwa kuwa kocha mkuu. (Football Insider).

Real Madrid wako katika kinyang'anyiro cha kumnunua beki wa Ujerumani Nico Schlotterbeck, 26, kutoka Borussia Dortmund kutokana na uhusiano wao wa kirafiki na klabu hiyo ya Bundesliga. (AS - Spanish).

Kocha wa Arsenal, Nicolas Jover, anapokea bonasi kila timu inapofunga kutokana na hali mbaya ya mpira. (Times - Subscription Required).

BBC

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
4m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
33m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’