Baada ya mchezo dhidi ya Simba uliopigwa visiwani Zanzibar na kumalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana, mabingwa watetezi wa ligi kuu ya NBC Yanga wanaeleka mkoani Singida ambako wanakabiliwa na mechi nyingine ngumu.
March 05 Yanga itakuwa dimba la Airtel huko Singida kuikabili Singida Black Stars katika mchezo mwingine unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali.
Katika mchezo uliopita dhidi ya Simba, wengi wanaamini Yanga haikuonyesha ubora wake pengine watahitaji kuzinduka huko Singida kuepuka kipigo kutoka kwa walima alizeti ho.
Mwezi huu Yanga, Simba, Azam Fc na Singida BS zitakuwa na mfululizo wa mechi za viporo zikiwa nyuma kutokana na ushiriki wao wa mashindano ya CAF.
Baada ya mchezo huo Wananchi watarejea Dar es salaam kuikabili Polisi Tanzania kwenye mchezo wa kombe la CRDB hatua ya 32 bora unaotarajiwa kupigwa uwanja wa KMC Complex March 08.
March 12 Yanga itakuwa Mbeya kumenyana na Tanzania Prisons kisha kurejea jijini Dar es salaam kumenyana na Azam Fc March 15.
March 18 huenda ikasafiri mkoani Arusha kuikabili TRA United ambayo imetangaza rasmi kuhamia mkoani humo. Baada ya mchezo huo Yanga itaelekea mkoani Dodoma kuikabili Mtibwa Sugar March 21.