Bado tuko kwenye mbio za ubingwa - Magori

Joel JJ By Joel JJ β€’ 3rd March 2026


Bado tuko kwenye mbio za ubingwa - Magori

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Crescentus Magori amesema dhamira ya Wekundu hao wa Msimbazi msimu huu ni kuwania ubingwa wa ligi kuu.

Magori amewataka mashabiki na wanachama wa timu hiyo kuunga mkono uongozi wao katika mapambano ya kurejesha heshima yao kwenye soka la ndani.

Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Yanga uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar juzi na kumalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana, Magori aliwapongeza wachezaji wa Simba kwa kuonyesha kiwango kizuri katika mchezo huo ambao anaamini walistahili kupata ushindi.

"Sisi tuko imara na tunapigania ubingwa, Wanasimba wote tuache fitna na ugomvi hii timu itakuwa nzuri zaidi ya hapa ilipo."

"Mechi zetu zinakuwa ngumu sana lakini ni mechi za ukweli, mechi za halali na hazina maigizo. Tutaendelea kucheza hivyo," alisema Magori.

Suluhu dhidi ya Yanga imeendelea kuiweka Simba katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakifikisha alama 24.

Simba tayari imerejea jijini Dar kujiandaa na mechi zinazofuata ambapo March 08 watacheza mechi ya hatua ya 32 bora kombe la CRDB dhidi ya B19 itakayopigwa uwanja wa Isamuhyo.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.