Klabu ya Singida BS imetangaza kumsamehe kiungo wake Mganda Khalid Aucho baada ya mchezaji huyo kuomba radhi.
Aucho alikuwa akitumikia adhabu ya kusimamishwa kwa miezi mitatu kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu.
Taarifa iliyotolewa na Singida BS mapema leo imebainisha kuwa Kamati ya nidhamu imemsamehe Aucho baada ya kukiri na kuomba radhi.




