Local,Normal News,Yanga, Azam, Singida, Prisons

Yanga kuikabili Singida BS bila Job, Azam Fc bila Fei Toto mikononi mwa Tanzania Prisons

Joel JJ By Joel JJ
β€’
5 Mar 2026
Yanga kuikabili Singida BS bila Job, Azam Fc bila Fei Toto mikononi mwa Tanzania Prisons

Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mechi mbili zinatarajiwa kupigwa mkoani Singida na Mbeya.

Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga wako Singida majira ya saa 10 jioni wakitarajiwa kushuka uwanja wa Airtel kuwakabili wenyeji wao Singida Black Stars katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali.

Katika mchezo huo Yanga itamkosa nahodha wake msaidizi beki Dickson Job ambaye alipata majeraha ya goti kwenye mchezo uliopita dhidi ya Simba.

Mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves pia jana alithibitisha kukosekana kwa Pacome Zouazoua na Edmund John wote wakiwa wanakabiliwa na changamoto za majeraha.

Mchezo mwingine unatarajiwa kupigwa mkoani Mbeya ambapo wenyeji Tanzania Prisons wataikaribisha Azam Fc.

Prisons wametoka kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Simba wakati Azam Fc walilamisishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Pamba Jiji katika mchezo uliopita.

Azam Fc leo watamkosa kiungo wao fundi Feisal Salum ambaye anatumikia adhabu ya kukosa mechi mbili baada ya kadi nyekundu aliyopewa kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
5h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
8h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
10h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
12h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
14h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
15h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
15h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
20h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’