International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa March 06 2026

Joel JJ By Joel JJ
β€’
6 Mar 2026
Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa March 06 2026

Manchester City wanakaribia kukamilisha dili la kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Elliot Anderson kutoka Nottingham Forest. (TeamTalks).

Anderson anapendelea kuhamia City zaidi ya majirani zake Manchester United, lakini Nottingham Forest wanamthamini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa zaidi ya Β£70m. (Sportsport).

Arsenal, Manchester United na Chelsea wako tayari kupigana vikumbo kumsajili beki wa kati wa England chini ya miaka 19 Samuel Amissah, 18, kutoka Fulham. (Telegraph - Subscription Required).

Liverpool wanamtaka Yan Diomande, 19, kuchukua nafasi ya Mohamed Salah katika wingi ya kulia na winga huyo wa RB Leipzig anaweza kuwagharimu pauni milioni 87. (TeamTalks)

Kocha wa zamani wa Spurs, Mauricio Pochettino na Roberto de Zerbi ndio walengwa wakuu wa Tottenham msimu huu wa joto - hata hivyo mchezaji wa zamani Robbie Keane, ambaye sasa anainoa Ferencvaros, anaweza kuzingatiwa ikiwa watashushwa daraja kwenye Ubingwa. (GiveMeSport).

Nafasi ya Arne Slot kama kocha wa Liverpool inatazamiwa kuchunguzwa sana mwishoni mwa msimu huu, huku kocha wa zamani wa Real Madrid Xabi Alonso akiwa ndiye meneja pekee ambaye wamiliki wa klabu hiyo wanataka kumrithi Mholanzi huyo. (TeamTalks).

Beki wa Ecuador Piero Hincapie, 24, atajiunga na Arsenal kwa uhamisho wa kudumu kutoka Bayer Leverkusen mwishoni mwa msimu huu. (Sun).

The Gunners watahitaji kumuuza mchezaji wa kikosi cha kwanza msimu huu wa joto, huku kiungo wa kati wa Norway Martin Odegaard, 27, na winga wa Brazil Gabriel Martinelli, 24, wakiwa miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa. (Telegraph - Subscription Required).

Manchester United inapanga kufanya mazungumzo ya kandarasi na kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 31, baada ya Kombe la Dunia msimu huu wa joto. (Football Insider).

Chelsea na Manchester City ni miongoni mwa vilabu vinavyomhitaji kiungo wa kati wa Bayern Munich na Ujerumani Aleksandar Pavlovic, 21, ambaye anaweza kugharimu euro 65m (Β£56m). (Ameotea).

BBC

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
6h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
10h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
11h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
13h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
16h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
16h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
16h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
18h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
22h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’