Local,Normal News,Yanga, Simba, Dodoma

Mwalimu afungiwa mechi tatu, Kamati yashusha adhabu kwa timu, wachezaji

Joel JJ By Joel JJ
β€’
6 Mar 2026
Mwalimu afungiwa mechi tatu, Kamati yashusha adhabu kwa timu, wachezaji

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Machi 4, 2026 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatayo;

Mechi Namba 133: Dodoma Jiji FC 3-0 TRA United FC

  • TRA United FC: Imepewa Onyo Kali kwa kosa la kikosi chake kuchelewa kufika uwanjani (saa 11:41 jioni badala ya saa 11:30 jioni).

  • Dodoma Jiji FC: Imetozwa faini ya Sh. 5,000,000 kwa kosa la meneja wa timu kutovaa sare za timu kama maofisa wengine.

  • Wachezaji Andy Lobulka Bikoko (Dodoma Jiji), Muhsin Malima Makame na Mzamiru Yassin Said (TRA United): Wametozwa faini ya Sh. 500,000 kila mmoja kwa kuchelewa kuingia uwanjani makusudi ili kukwepa kupeana mikono na waamuzi na wapinzani.

  • TRA United FC: Imetozwa faini ya ziada ya Sh. 5,000,000 kwa kushindwa kuwasilisha orodha ya viongozi wa benchi la ufundi.

Mechi Namba 080: Namungo FC 0-1 Young Africans SC

  • Mwamuzi Abdallah Mwinyimkuu (Singida): Ameshushwa daraja kwa makosa ya kujirudia ya kushindwa kutafsiri sheria, ikiwemo kutochukua hatua mchezaji Abdulkarim Kiswanya (Namungo) alipovutwa jezi na Mussa Damaro (Yanga) ndani ya eneo la penati.

  • Adhabu ya awali: Mwamuzi huyu pia alikuwa ameshaadhibiwa mwezi Desemba 2025 kwa kuondolewa kwenye orodha ya waamuzi kwa mizunguko mitano (5) kwa makosa ya aina hiyo.

Mechi Namba 077: Dodoma Jiji FC 0-0 Simba SC

  • Seleman Mwalimu (Simba SC): Amefungiwa michezo mitatu (3) na faini ya Sh. 1,000,000 kwa kumpiga kiwiko kwa makusudi mchezaji Andy Lobulka Bikoko.

  • Simba SC: Imetozwa faini ya Sh. 5,000,000 kwa kosa la mashabiki wake kumrushia chupa za maji mchezaji William Edgar wa Dodoma Jiji na wahuduma wa kwanza (Redcross).

  • Dodoma Jiji FC: Imetozwa faini ya Sh. 5,000,000 kwa kosa la wahuduma wake wa kwanza (Redcross) kuonekana wakichelewa kuingia uwanjani kwa makusudi ili kupoteza muda.

  • Mwamuzi wa Akiba Charles Simon (Dodoma): Amefungiwa miezi mitatu (3) kwa kuruhusu Dodoma Jiji kufanya mabadiliko ya wachezaji katika mikupuo minne (4) badala ya mitatu (3).

  • Dodoma Jiji FC: Imetozwa faini nyingine ya Sh. 5,000,000 kwa kufanya mabadiliko hayo ya wachezaji katika mikupuo minne (4) kinyume na kanuni.

  • Abdi Banda (Dodoma Jiji FC): Amefungiwa michezo mitatu (3) na faini ya Sh. 1,000,000 kwa kukataa kutoka uwanjani kwenye machela baada ya kupata maumivu ili kupoteza muda.

Mechi Namba 054: Young Africans SC 0-0 Simba SC

  • Simba SC: Imetozwa faini ya Sh. 5,000,000 kwa kuingia uwanja wa Amaan (Zanzibar) kupitia mlango usio rasmi.

  • Simba SC: Imetozwa faini nyingine ya Sh. 5,000,000 kwa kukataa kutumia chumba rasmi cha kuvalia na kutumia chumba cha mikutano ya wanahabari.

  • Simba SC na Young Africans: Klabu zote mbili zimetozwa faini ya Sh. 5,000,000 kila moja baada ya walinzi wao kugombana na kutoleana lugha ya matusi wakati Simba ikiwasili uwanjani.

  • Simba SC: Italazimika kulipa gharama za matengenezo ya mlango wa chumba cha mikutano ya wanahabari uliovunjwa na walinzi wao.

  • David Kameta (Simba SC): Ametozwa faini ya Sh. 1,000,000 kwa kuonekana akimwaga kimiminika kiwanjani, kitendo kilichotafsiriwa kama imani za kishirikina.

  • Mwamuzi Msaidizi Namba 1 Kassim Mpanga (Dar es Salaam): Amefungiwa miezi sita (6) kwa kukataa bao halali la Simba (dakika ya 70) kwa madai ya kuotea, jambo ambalo video ilithibitisha hakuwa ameotea.

  • Mwamuzi Msaidizi Namba 2 Hamdan Said (Mtwara): Amefungiwa miezi mitatu (3) kwa kuashiria mchezaji Prince Dube (Yanga) alikuwa ameotea (dakika ya 61) na kusimamisha shambulizi, wakati hakuwa ameotea.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’