Yanga yahoji kanuni iliyotumika kumfungia mshambuliaji Simba

Joel JJ By Joel JJ • 7th March 2026


Yanga yahoji kanuni iliyotumika kumfungia mshambuliaji Simba

Klabu ya Yanga imewaandikia barua kw Bodi ya Ligi, ikihitji ufafanuzi wa kina juu ya adhabu iliyotolewa na Kamati ya saa 72 kwa mchezaji wa Simba Selemani Mwalimu.

Akizungumza ktika mkutano na wanahabari mapema leo Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alisema kuwa klabu hiyo imewasilisha barua rasmi baada ya kubaini kile walichokiita kuwa ni utofauti wa kikanuni katika kushughulikia makosa yanayofanana.

Kamwe amebainisha kuwa, wakati wachezaji wengine watano msimu huu walifungiwa mechi tano kwa makosa ya aina hiyo chini ya kanuni ya 41:21, Mwalimu amepewa adhabu ya mechi tatu pekee kwa kutumia kanuni ya 41:5(5.2).

Yanga imeitaka Bodi iweke wazi 'upekee' wa tukio la mchezaji huyo ulioifanya Kamati ya saa 72 kulegeza adhabu hiyo tofauti na msimamo uliochukuliwa kwa wachezaji wengine waliotangulia.

“Tumewaandikia barua Bodi ya Ligi, tukihitaji kupata ufafanuzi wa kina juu ya adhabu iliyotolewa na Kamati ya saa 72 kwa mchezaji Selemani Mwalimu. Msimu huu wachezaji watano wamefungiwa mechi 5 kwa kosa linalofanana na Mwalimu, lakini yeye amefungiwa mechi 3."

"Tunahitaji Bodi iweke bayana kuna upekee gani wa tukio la Mwalimu lililoifanya Kamati ya saa 72 kutumia kanuni tofauti ya 41:5(5.2) na wengine watano kutumika kanuni ya 41:21.”

“Jambo la pili, tumeitaka Bodi ya Ligi itoe ufafanuzi kwanini kamati ya saa 72 ilichelewa kukutana kama kanuni zinavyoelekeza ili kufanya mapitio ya makosa mbalimbali na kutoa hukumu kwa waliobainika ikiwemo tukio la mchezaji Selemani Mwalimu."

"Aidha mechi zingine zilizopita Kamati hii ya saa 72 ilikutana kwa wakati na kutoa hukumu. Kulikuwa na changamoto gani iliyopelekea kucheleweshwa kwa haki,”alisema Kamwe


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.