Local,Normal News,Yanga, Prisons

Nsajigwa aipigia hesabu kali Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
8 Mar 2026
Nsajigwa aipigia hesabu kali Yanga

Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons Shadrack Nsajigwa amesema malengo ya kikosi chake ni kuhakikisha wanaendelea kufanya vyema kwenye ligi kuu ya NBC ili kujiepusha na hatari ya kuteremka daraja.

Nsajigwa alianza vyema majukumu yake ya kuinoa Prisons akifanikiwa kuondoka na alama moja katika mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc.

Mchezo unaofuata kwa Prisons ni dhidi ya mabingwa watetezi Yanga ambao watakutana nao Alhamisi, March 12 katika uwanja wa Sokoine.

Nsajigwa aliyewahi kuwa na nahodha wa Yanga, amesema kuelekea mchezo huo wanatambua ugumu ulio mbele yao lakini dhamira yake ni kuona kikosi chake hakipotezi mchezo huo.

"Tunajua ugumu wa Yanga, ni timu kubwa na wachezaji wazuri, lakini tunaenda mechi kwa mechi. Kila mchezo kwetu ni vita ya pointi ili tujiweke salama kwenye msimamo," alisema Nsajigwa

Kabla ya mchezo dhidi ya Yanga, Tanzania Prisons leo watashuka dimbani wilayani Chunya kuvaana na TMA katika Kombe la Shirikisho la CRDB (Hatua ya 32 bora).

Yanga pia itashuka dimba la KMC Complex kuikabili Polisi Tanzania kwenye mchezo wa kombe la CRDB

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’