Klabu ya Simba imethibitisha kumuongezea mkataba kiungo wa kati Yusuph Kagoma.
Kagoma ameongeza mkataba wa miaka miwili kuwatumikia Wekundu hao wa Msimbazi. Mkataba wake awali ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu.
Ni hatua ya nzuri kwa uongozi wa Simba kumuongezea mkataba mapema kiungo huyo mkabaji ambaye kwa sasa ni moja ya nguzo ya Simba katika eneo la kiungo.


Simba pia imemuongea mkataba beki raia wa Afrika Kusini, Rushine de Reuck.
Rushine ameongeza mkataba wa mwaka mmoja Simba ikitumia kipengele kilichowekwa kwenye mkataba wake wa awali.
Beki huyo ambaye ni mmoja wa manahodha wa Simba alitua Msimbazi kwa mkopo wa mwaka mmoja kutoka klabu ya Mamelodi Sundowns mkataba wake ukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mwingine kama Simba itaridhishwa na uwezo wake.
Uongozi wa Simba umeweka mkakati wa kuhakikisha nyota wote muhimu kwenye kikosi cha kwanza wanakuwa na mikataba ya muda mrefu.